Social Icons

Featured Posts

Thursday, October 9, 2014

TAARIFA KWA WANAFUNZI WA CHUO CHA AFYA.
SELIKARI YA WANAFUNZI CHUO CHA AFYA INAWATANGAZIA WANAFUNZI WOTE KUWA GHARAMA ZA MALIPO YA DIRECT COST YATAKUWA KAMA YALIVYO KUWA KIPINDI CHA NYUMA, HII NI KUTOKANA NA TAARIFA  ILIYO TOLEWA TAREHE 9 SEPTEMBER ,2014, NA CHUO KUWA WANAFUNZI WOTE MNAOENDELEA MNATAKIWA KULIPA 461000/= BADALA YA 26500.
HII ILIPELEKEA MAZUNGUMZO YA HARAKA YAFANYIKE KUPITIA UONGOZI WA SERIKALI YA WANAFUZI, HIVYO BASI SERIKALI YA WANAFUNZI INAWATAALIFU WANAFUNZI WOTE KULIPA PESA HIYO KUPITIA ACCOUNT ZILOPO KWENYE WEBSITE YA CHUO, LAKIN PIA WANAFUNZI WENZANGU NIWASHUKURUNI SANA KWAN MLIONESHA UVUMILIVU JUU YA TAARIFA HII BASI MDUMU KATIKA HALI HII.

LAKIN PIA SERIKALI YA WANAFUNZI INAWATANGAZIA WANAFUNZI WOTE WENYE SUPPLEMENTARY, HUDUMA YA MAKAZI INAPATIKANA CHUON HAPO TOKA TAREHE 1 OCTOBER, 2014 KAMA ILIVYO TANGAZWA AWALI KUPITIA MAWASILIANO YA SIMU, HIVYO BASI KWA WALE MANAOHITAJI MUDA WA KUJIANDAA VYEMA HUKU WAKIWA CHUONI BASI WAFIKE CHUON HAPO ILA WATATAKIWA KULIPA KIASI CHA 500/= KWA SIKU PESA HII ILIPWE KENYE ACCOUNT YA CHUO KABLA YA KURIPORT,.
HOSTELI ZA EDUCATION HAZITA TUMIKA KATIKA MUDA HUU WA KUJIANDAA NA MITIHAN KULINGANA NA UTARATIBU MZIMA WA MATUMIZI WA HOSTELI HIZO KUCHUKUA MUDA, HIVYO BAS WANAFUNZI WOTE MFIKIE CoHS,.

Rais.


TANGAZO KWA UMMA
7 September, 2014

YAH: KUJIUZULU KWA KA TIBU MKUU WA 
SERIKALI YA WANAFUNZI NA KUVUNJWA KWA 
WIZARA YA MICHEZO NA HUDUMA ZA JAMII.
NDUGU WANAFUNZI WA CHUO CHA SAYANSI ZA AFYA NAPENDA
KUWATANGAZIA KUWA    OFISI YA RAIS ILIPOKEA BARUA YA KUJIUZULU
KUTOKA KWA KATIBU MKUU WA SERIKALI YA WANAFUNZI TAREHE
30/07/2014 IKIWA INATOA TAARIFA YA KUJIUZULU , SABABU KUU YA
KUJIUZULU NI KUSHINDWA KUWAJIBIKA IPASAVYO KATIKA NAFASI HII
HUKU AKIENDELEA NA SHUGHULI YA  MASOMO. HIVYO KWA MUJIBU WA
KATIBA YA UDOSO CHAPTER TWO,PART 1,14(4)b INAMP A MAMLAKA RAIS
KUTEUA KATIBU WA SERIKALI NA PIA CHAPTER TWO PART 1,16(5) KATIBA
INATOA MAELEKEZO JUU YA KUJIUZULU KWA KATIBU KUWA MOJA KWA
MOJA NAFASI HIYO INAKUWA WAZI PIA CHAPTER TWO, PART 1,16(6)(C)
KATIBA INAELEZA KUWA KATIBU ATASHIKILIA NAFASI YAKE MPAKA PALE
ATAKAPO JIUZULU. HIVYO BASI OFISI YA RAIS INAPENDA KUWATAARIFU
KUWA  MH SELEMANI MBANGULA KUANZIA    TAREHE 31/07/2014 YUKO
NJE YA OFISI
.
WIZARA YA MICHEZO NA HUDUMA ZA JAMII
NDUGU WANAFUNZI WENZANGU NAWATAARIFU KUWA WIZARA YA
MICHEZO IMEVUNJWA RASIMI TAR 7/08/2014.
HIVYO BASI:-
WAZIRI WA MICHEZO: MOSHA HENRY G.
NAIBU WAZIRI :MUSTAPHA ADAM
HAWATA KUWA VIONGOZI KATIKA WIZARA HII:
NDUGU WANAFUNZI    SABABU ZA KUVUNJWA KWA WIZARA HII NI KAMA
IFUATAVYO:
1;KUTOWEPO KWA MAELEWANO YA    
KIUTENDAJI BAINA YA VIONGOZI WA WIZARA    HII
IMESABABISHA WIZARA KUSHINDWA KUFANYA KAZI KWA UFANISI
UNAOTAKIWA.

2; KUSULUHISHWA KWA VIONGOZI KATIKA WIZARA HII MARA
KADHAA NA KUPEWA MWONGOZO WA KAZI BILA MAFANIKIO.

3;KUDHARAU MAAMUZI YA BARAZA LA MAWAZIRI YA TAREHE
18 JULAI 2014, JUU YA KUKUTANA NA VIONGOZI WA PANDE ZOTE
MBILI STASHAHADA MWAKA WA KWANZA NA SHAHADA MWAKA
WA KWANZA ILI KUTAFUTA SULUHU JUU YA VURUGU ZA MCHEZO
WA FAINALI MPIRA WA MIGUU, MBUZI CUP ,ILIO FANYIKA  JULAI
11 ,2014 .

4; KUJIUZULU KWA NAIBU WAZIRI KATIKA WIZARA HII, MNAMO
TAREHE 20 JULAI 2014, OFISI YA RAIS IMEPOKEA BARUA YA NAIBU
WAZIRI KATIKA WIZARA HII AKIMTAARIFU RAIS JUU  YA
KUSHINDWA KUENDELEA KUTUMIKIA UMMA KUPITIA WIZARA HII.
KUTOKANA NA SABABU 1,2,3,&5 ZILIZOTAJWA HAPA.

5; WIZARA KUSHINDWA KUWAKUTANISHA WADAU WA SOKA
KWA PAMOJA ILI KUPATA UTATUZI WA CHANGAMOTO ZA
KUTOKUELEWANA BAINA YA WADAU HAO;    IKUMBUKWE KUWA
HALI HII YAWEZA KUJENGA UHASAMA MKUBWA.NA KUVURUGA
HALI YA KIMICHEZO CHUONI KWETU

KWA HALI HII BASI;
KWA MUJIBU WA KATIBA YA SERIKALI YA WANAFUNZI YA MWAKA 2007
ILIYO FANYIWA MAREKEBISHO MWAKA 2009, CHAPTER TWO, PART I, 14 (4)(b)
INAMPA MAMLAKA RAIS YA KUCHAGUA WAZIRI AMA NAIBU WAZIRI
KATIKA WIZARA HUSIKA.
PIA SEHEMU YA KATIBA YA SERIKALI YA WANAFUNZI ,CHAPTER TWO , PART
I ,16F (3)(b), INAMPA RAIS MAMLAKA WA KUMWONDOA WAZIRI    AMA
NAIBU WAZIRI KUTOKA KATIKA WIZARA LAKINI PIA CHAPTER TWO,PART
I, 16F(3)(a) INAELEZA NAFASI YA KIONGOZI WA WIZARA YAWEZA BAKI WAZI
ENDAPO KIONGOZI WA WIZARA    AKIFA AU KUJIUZURU.
NIMEAMUA KUIVUNJA WIZARA HII NA KUUNDA UONGOZI MPYA AMBAO
UTAFANYA KAZI KWA KIPINDI KILICHO BAKI.
RAI YANGU KWENU WANAFUNZI WENZANGU, TUWE WATULIVU
TUDUMISHE AMANI YA CHUO CHETU ILI KUJENGA JAMII YENYE UPENDO
NA USHIRIKIANO/MSHIKAMANO    MZURI.
N.B MABADILIKO KATIKA WIZARA HII YATATANGAZWA .
IMETOLEWA NA;
…………………………..
MATHIAS RENATUS
Rais:- chuo cha afya

Saturday, August 9, 2014

WIZARA YA FEDHA NA USAFIRI-TANGAZO LA MALIPO YA UDOSO FEE 2014-2015

WIZARA YA FEDHA NA USAFIRI

WAZIRI:             MH, EDWARD SIMON

N/ WAZIRI: MH. SALOME J. MWALUKIMBA












TANGAZO KWA WANAFUNZI WOTE WA CHAS

 CHUO KIKUU CHA DODOMA (UDOSO CHAS)

TAMKO LA WIZARA YA FEDHA NA USAFIRI


NDUGU WANAFUNZI WA CHAS KWANZA KABISA NAOMBA NIWAPE POLE KWA MAANDALIZI YA MITIHANI YA KUFUNGA NA KUHAMA MWAKA.
KUTOKANA NA KATIBA YA UDOSO IBARA YA 3 SEHEMU YA KWANZA KIFUNGU KIDOGO CHA 22(1) INATOA MAMLAKA KWA SERIKALI ZA VITIVO KUKUSANYA MAPATO YAKE YENYEWE NA NDO MFUMO UNAOTUMIWA NA SERIKALI ZA VITIVO VINGINE.
KWAHIYO  WIZARA INAPENDA KUWATAARIFU  WANAFUNZI WOTE KUWA MALIPO YA MICHANGO KWA AJILI YA UENDESHAJI WA SERIKALI YA WANAFUNZI(CHAS) YALIPWE KUPITIA ACCOUNT YETU YA CHAS ILI KUEPUKA USUMBUFU UNAOJITOKEZA KUHAMISHA FEDHA KUTOKA ACCOUNT YA FEDERAL KWENDA ACCOUNT YA CHAS.
A/C NO.0150221581000
A/C DESCRIPTION:UDOSO CHAS
BRANCH:CRDB BANK
AMOUNT:TSH 5,000/=

MWISHO WIZARA INAPENDA KUWASISITIZA WANAFUNZI WANAOENDELEA NA MASOMO(CONTINUING)KUWAKUMBUSHA NDUGU ZETU WATAKAOJIUNGA NA MWAKA WA KWANZA(2014/2015)KULIPIA PESA HIYO KUPITIA A/C NO HIYO ILI KUEPUKANA NA USUMBUFU UTAKAOJITOKEZA KIMSINGI  WIZARA HAITATAMBUA MALIPO YOYOTE YATAKAYOLIPWA KWENYE A/C ZINGINE ZAIDI YA LILYOTAJWA HAPO JUU. 

Friday, August 8, 2014

SERIKALI MPYA YA WANAFUNZI CHAS 2014-2015

AWALI YA YOTE NAPENDA KUMSHUKURU MUNGU KWA UZIMA NA AMANI TULIO NAYO KITIVONI KWETU LAKINI PIA NIWASHUKURU WANAFUNZI WOTE KWA KUNIAMINI NA KUNIPA RIDHAA YA KUWA MWAKILISHA KATIKA MAJUKUMU MBALIMBALI KUPITIA CHOMBO CHA SERIKALI YA WANAFUNZI KUWA KAMA RAIS WAO. NAWAHAIDI KUYAFANYA YOTE MEMA NINAYO PASWA KUFANYA. IKUMBUKWE KUWA HAKUNA KIONGOZI IMARA BILA WATU IMARA HIVYO NAWAOMBENI NDUGU ZANGU TUSHIRIKIANE KWA PAMOJA KUNIFANYA MIMI KUWA KIONGOZI IMARA KWA MCHANGO WENU WA MAWAZO NA MAOMBI.

KUFUATIA UCHAGUZI ULIO FANYIKA TAREHE 21/04/2014 WAFUATAO WALICHAGULIWA  KUIONGOZA SERIKALI YA WANAFUNZI CHAS:-      

RAIS WA SERIKALI YA WANAFUNZI






"ukweli haupo sehemu unasuburi ugunduliwe lakini ukweli unatengenezwa"







MH. MATHIAS RENATUS

MAKAMU WA RAIS SERIKALI YA WANAFUNZI












MH. VICTORIA LYIMO

BAADA YA UCHAGUZI ZIFUATAZO NI NYAZIFA ZA JUU ZA SERIKALI ZA KUTEULIWA NA MH. RAIS.

WAZIRI MKUU SERIKALI YA WANAFUNZI




"ili kujenga jamii endelevu na yenye mafanikio ni lazima kuwashinda maadui wakuu wafuato:- ubinafsi,uzembe na uvivu wa kufikiri."










MH. SOLOMON SAMWEL

NB:- baraza la mawaziri na viongozi wengine mbalimbali taarifa zao zitawekwa siku si nyingi.


Thursday, June 5, 2014

TAARIFA YA MAKABIDHIANO YA UONGOZI 01/06/2014.

CHUO KIKUU CHA DODOMA
KITIVO CHA SAYANSI YA AFYA NA TIBA
SEREKALI YA WANAFUNZI (UDOSO-COHS)
OFISI YA KATIBU MKUU WA KITIVO 2013/2014
TAARIFA YA MAKABIDHIANO YA UONGOZI 01/06/2014.
1  UTANGULIZI
Awali ya yote serikali inapenda kumshukuru Mwenyezi Mungu kwa fadhili zake kwetu kwani ametulinda salama tangu pale tulipokabidhiwa uongozi mpaka sasa tunapofikia tamati ya kipindi chetu cha uongozi. Shukrani za dhati pia ziende kwa watangulizi wetu serikali iliyokuwa chini ya Raisi mstaafu Adam Mandala pamoja na Baraza lake la Mawaziri. Aidha hatuwezi kusahau ushirikiano mathubuti tulioupata toka kwa Uongozi wa Chuo kuanzia Utawala Mkuu na katika ngazi ya College pamoja na Bodi ya Mikopo (HESLB).

PICHA ZA VIONGOZI WASTAAFU UDOSO-CHAS(2013-2014)

HON. ABAYO ASUBUHI; THE PRESIDENT 2013-14




 PETRO MATHIAS, VICE PRESIDENT 2013-14

Friday, January 31, 2014

                                    


THE NEW ANNOUNCEMENT TO ALL STUDENTS, COLLEGE OF HEALTH SCIENCES,
UNIVERSITY OF DODOMA, CONCERNING FINANCES FOR SPECIAL FACULTY, BOOKS & STATIONARY, AND COMMUNITY FIELD MD4; BOTH GRANT AND LOAN.