CHUO
KIKUU CHA DODOMA
KITIVO
CHA SAYANSI YA AFYA NA TIBA
SEREKALI
YA WANAFUNZI (UDOSO-COHS)
OFISI
YA KATIBU MKUU WA KITIVO 2013/2014
TAARIFA
YA MAKABIDHIANO YA UONGOZI 01/06/2014.
1 UTANGULIZI
Awali
ya yote serikali inapenda kumshukuru Mwenyezi Mungu kwa fadhili zake kwetu
kwani ametulinda salama tangu pale tulipokabidhiwa uongozi mpaka sasa
tunapofikia tamati ya kipindi chetu cha uongozi. Shukrani za dhati pia ziende
kwa watangulizi wetu serikali iliyokuwa chini ya Raisi mstaafu Adam Mandala
pamoja na Baraza lake la Mawaziri. Aidha hatuwezi kusahau ushirikiano mathubuti
tulioupata toka kwa Uongozi wa Chuo kuanzia Utawala Mkuu na katika ngazi ya College
pamoja na Bodi ya Mikopo (HESLB).
Shukrani
za pekee tunazitoa kwa Mkuu wa Chuo cha Afya Prof A. Gessase, Wakuu wa schools
Dr. I. Mwapagatwa na Dr. M. Mwashambwa, Loan Officer CoHS, na wakuu wote wa Maidara
bila kuwasahau Prof. Msofe (Director of undegraaduate studies), Mshauri Mkuu wa
Wanafunzi, Dick N. Manongi na Makamu Mshauri wa wanafunzi Madam Rhoda Aroko kwa
ushirikiano wao kwetu katika kipindi chote cha uongozi bila kusitasita pale
tulipo hitaji msaada wao.
Mwisho
tunawashukuru wanafunzi kwa kutuamini na kutupa ridhaa ya kuwaongoza kwa
kipindi chote cha uongozi. Kweli hatutasahau fadhila zao kwetu, na hii
imetusababisha serikali kufanya kila lililowezekana kushughulikia matatizo yao
kwa uaminifu, uadilifu, kwa wakati na kwa njia ya amani.
Mwenyezi
Mungu ambariki kila Mtu sawasawa na Fadhili zake.
Taarifa hii imegawanyika katika sehemu kuu tano ambazo ni
1. Utangulizi,
2. Malengo
3. Mafanikio
4. Changamano
5. Taarifa
ya mapato na matumizi
6. Mapendekezo
na Hitimisho
2. MALENGO
Serikali hii
ilijumuisha Wizara sita (6), ambazo ni Wizara ya elimu, Wizara ya mikopo, Wizara
ya fedha katiba sheria na utawala bora,
Wizara ya afya na chakula, Wizara ya michezo na nahusiano ya jamii na Wizara ya
makazi, umeme na maji. Hiyvo kupitia Wizara hizi serikali ilipanga kufanya
fafuatayo.
NB: Malengo haya
yameelezwa kwa ufupi sana kwa ufafanuzi rejea taarifa za serikali husika.
v Kushughulikia
mikopo katika Nyanja zake zote kama ambavyo imeelezwa katika taarifa ya Wizara husika
v Kushughulilikia
taaluma katika Nyanja zake zote kwa wanafunzi wote.
v Kuhakikisha
upatikanaji wa makazi bora kwa wanafunzi wote.
v Kuhakikisha
upatikanaji wa huduma za kiafya kwa wanafunzi wote na kufatilia kwa karibu
upatikanaji wa kadi za bima ya afya, chakula bora, na mazingira masafi ambayo
yangesaidia kuzuia kutokea kwa magonjwa ya mlipuko.
v Kuhakikisha
ukusanyaji na matumizi stahiki ya fedha za UDOSO
v Kuelimisha
jamii na kuhakikisha upatikanaji wa nakala za rasimu ya katiba ambayo ilikuwa
katika mchakato wa kuandaliwa.
v Kuhakikisha
mazingira sahihi na salama ya kusoma kwa vitendo kwa wanafunzi wanaoenda katika
Hospitali za Tumbi na Iringa, na Wanafunzi wanaotumia Hospitali za Dodoma.
v Kuendeleza
na kuboresha Michezo na Burudani kwa kushiriki katika michezo mbalimbali na
kununua vifaa vya michezo kwa michezo tuliyo nayo.
3.
MAFANIKIO
Mafanikio haya yameelezwa kwa ufupi kuzingatia yale
yaliyofanywa na wizara husika. Taarifa za wizara zina maelezo ya ziada.
A.Wizara Ya
Mikopo
Ø Serikali
imefanikiwa kufuatilia kwa karibu na kufanikisha wanafunzi 13 wa mwaka wa
kwanza 2012/13 ambao hawakuwa na mikopo, kupata mikopo.
Ø Serikali
imefanikiwa kupatikana kwa fedha za field na Research kwa wanafunzi katika
kipindi chote uongozi. Kama ifuatavyo;
o
BSc MW(4), BScN 4 , MD2 2012/13, MD3
2012/13
o
MD4 2012/13, MD4 2013/14, MD5 2013/14.
Ø Tumefanikiwa
kuwaunganisha wanafunzi 76 wa MD1 (2012/13) wenye sifa stahiki kupata grants
toka serikalini. Sambasamba na hilo
serikali imefanikiwa kuendeleza mchakato wa kuwaunganisha wanafunzi wa MD1
(2013/14) katika grants na mpaka sasa wote wenye vigezo wamesaini fomu za
kujiunga hivyo ni matarajio yetu kuwa wataingizwa katika mfumo kuanzia mwaka
ujao wa kimasomo kama ilivyo utaratibu wa serikali.
Ø Serikali
imefanikiwa kufuatilia kwa karibu madeni ya ADA ya miaka ya nyuma na mwaka huu
wa masomo. Jambo hili limefanikiwa kwa kiasi kikubwa sana kwani kwa madai ya
nyuma ni wanafunzi wachache sana (‹5) ndio wenye madai. Pia kwa wanafunzi wenye
mikopo karibia wote wameshalipiwa ADA, waliobaki ni wachache tu hasa ambao wana
matatizo ya mikopo hata hivyo, maombi ya fedha hizo yalishatumwa HESLB kwa
ajili ya utekelezaji zaidi.
Ø Serikali
imefanikiwa kufanya juhudi zilizosaidia kurejeshwa kwa mikopo ya wanafunzi
ambao mikopo yao ilipelekwa vyuo vingine na mpaka sasa wanapata mikopo yao na
wale ambao wanamadai serikali inaendelea kushughulikia matatizo yao.
Ø Serikali
imefanikiwa kupata taarifa ya mabadiliko ya kufanya –Upadate ya mikopo kama
ilivvokuwa ikifanyika kila mwaka hapo hawali. Kuwa kwa mwaka huu hakuna
ku-update isipokuwa wanafunzi watapewa mikop yao kulingana na taarifa ya
matokeo toka chuoni. Pia kwa waliohairisha mwaka na wenye malipo pungufu
watafanyiwa amarekebisho kutokana na matokeo yao ya mwisho wa mwaka.
Katika wizara ya Afya,
Serikali imefanikiwa kufanya yafuatayo.
Ø Wizara
imefanikiwa kuhakikisha upatikanaji wa huduma ya chakula kwa wakati. Kwani hapo
awali iliwachukua wanafunzi muda mrefu katika foleni, hali hii ilisababishwa na
uchache wa wagawaji na meza za kugawia vyakula (bufee). Lakini kwa sasa wahudumu
na huduma imeboreshwa.
Ø Wizara
imefanikiwa kudhibiti bei ya vyakula pamoja na vinywaji. Serikali imefanikiwa
kudhiti bei ya vinywaji pia, kwani katika kitivo cheti, ndiyo kitivo pekee
ambapo vinywaji vinapatikana kwa bei ya chini ukilinganisha na vitivo vingine.
Ø wizara
pia imefanikiwa kuhakikisha upatikanaji wa huduma kwa wanafunzi wote waliougua
ghafla hasa wakati wa usiku. Hawa wanafunzi wote waliougua waliitiwa gari la
wagonjwa kuwapeleka katika kituo cha afya na pale ambapo usafiri ulikosekana
serikali ilitoa gharama ya kukodi gari kuwapeleka hospitalini.
Ø Sambamba
na hayo, wizara imefanikiwa kufuatilia kwa karibu na kuwawezesha wanafunzi
kupata kadi za bima za afya NHIF-card.
C: Mafanikio Ya Wizara Ya Makazi, Maji Na Umeme.
Ø Wizara imefanikiwa kuhakikisha kuwa kila mwanafunzi
wa CoHS anapata makazi bora, na salama, ikiwa ni pamoja na Wanafunzi wa Tumbi
na Iringa. Hii ni pamoja kufanikiwa kuwapatia makazi ya pamoja wanafunzi wanaoishi katika chuo cha Elimu (CoED) kuishi block D,G
na F. Pia wanafunzi wa Iringa na Tumbi wana makazi ya uhakika.
Ø
Wizara
imejitahidi kuwasiliana na utawala kuhusiana na ukarabati wa njia za maji
bafuni na ukarabati wa mabweni kwa ujumla na wamekuwa wakifanya
ukarabati hatua kwa hatua ingawa bado haujakamilika.
Ø Wizara imefanikiwa kuhakikisha kuwa maji safi na
umeme vinapatikana na kutoa taarifa mapema pindi hitilafu ya maji au umeme
inapoatokea, na wakati maji yalipokosekana kabisa, jitihada nyingi zilifanywa
kuhakikisha maji yanaletwa na gari
Ø Wizara imefanikiwa kuweka vikao kadhaa ili kutoa
elimu na kujadiliana na wanafunzi na wardens juu ya hali ya utunzaji wa
mabweni.
Ø Upatikanaji wa maji safi kwa wanafunzi wanaoishi
education umekuwa ukisumbua lakini wizara imekuwa ikiwasiliana mara kwa mara na
mafundi wa maji panapotokea uhaba wa maji.
Ø Wizara imefanikiwa kuwapokea wanafunzi wa mwaka wa
kwanza ikiwa ni pamoja na kuwapatia magodoro na maelekezo muhimu.
D.
Mafanikio
Ya Wizara Ya Elimu.
Ø Wizara
imefanikiwa kuendelea kujenga mahusiano mazuri kati ya utawala, waalimu, watumishi
wa maktaba jambo ambalo limesaidia kurahisisha upatikanaji wa huduma bora na
kwa wakati.
Ø Wizara
imefanikiwa kufahamisha mambo mengi yahusikayo na taaluma ikiwa ni pamoja na kanuni
za mitihani kwa kuwapatia prospectus na
kitabu cha kanuni za mitihani
(examination regulations books).
Ø Symposium: wizara kwa kushirikiana na utawala imefanikiwa
kuendesha symposiums , ambazo zimesaidia wanafunzi kukua kitaaluma, kwani mada
mbalimbali zilijadiliwa kuhusiana na taaluma yetu.
Ø Upatikananaji
wa Lecturers And Clinical Instructors. Katika kipindi cha uongozi tumefanikiwa
kupata waalimu wa nje kwa masomo yale ambayo hayana waalimu pia tumefanikiwa
kutatua tatizo la waalimu wa kutuelekeza kwa njia ya vitendo pale tunapokwenda
hospitalini kwa ajili ya mafunzo kwa vitendo.
Ø Serikali
imefanikiwa kutambua na kushughulikia changamoto zinazojitokeza siku kwa siku
katika masomo na mitihani, ambapo vikao vimefanyika kati ya Wanafunzi na Serikali na kati ya
wanafunzi, Serikali na Uongozi wa Chuo cha Afya ili kupata suluhisho juu ya
Changamoto hizo.
E. WIZARA YA MICHEZO NA MAMBO
YAKIJAMII
1.
Serikali ilifanikiwa kuendesha Bonanza
mbalimbali mfano Vodacom, na PPF bonanza na UDOM intercollege Bash. Pia kuendesha
Mechi mbalimbali za Kirafiki kama vile mechi za ki-madarasa, kozi, mechi kati
ya CoHS na chuo cha veta, na ng’ong’ona. Chini ni orodha ya Mechi zilizochezwa;
·
Mwaka wa I&II
·
Skuli ya Uuguzi na Skuli ya Udaktari
·
TAMSA VS UNSATA
·
Wanafunzi wa Shahada na wa stashahada
·
UDOM staff na Timu ya wanafunzi CoHS
·
CoHS na HUMANITY
·
CoHS na COED
·
CoHS na VETA
·
CoHS na WAJASIRIAMALI Ng’ong’ona.
2.
Serikali imefanikiwa kuweka huduma za
DSTV zinazopatikana wakati wote katika makazi ya Wanafunzi Block F kwa
wanafunzi wanaokaa chuo cha Elimu na kuhakikisha upatikanaji wa huduma hiyo
katika Cafetereia ya CoHS kwa wanafunzi wanaokaa CoHS.
3.
Serikali imefanikiwa kuhamasisha
wanafunzi wengi kushiriki michezo mbalimbali.
4.
Serikali imefanikiwa kupata vifaa vya
michezo ambavyo ni mipira,filimbi, pampu, net, na jersey kwa kipindi chote cha
uongozi.
5.
Serikali imeanzisha timu za netball, and
basketball ambazo hazikuwepo hapo mwanzo.
6.
Serikali ilifanikiwa kuandaa wachezaji
walioshiriki michezo mbalimbali wakati wa michezo ya TUSA na kufanikiwa kuletea
UDOM ushindi, kwa kupata mshindi wa I na wa II katika mchezo wa table tennis
kutoka CoHS.
7 Sambamba na hilo pia, Serikali
ilifanikiwa kutuma Wachezaji 4 wa Mpira wa miguu nje ya Chuo kwa ajili ya
kushiriki TUSA Sport tour.
8 Serikali ilifanikiwa kufanikisha UDOM Intercollege
Bash katika chuo cha CIVE.
9 Serikali imehakikisha uwepo wa usafiri muda wote kutoka chuo cha Elimu
kwenda chuo cha Afya na wakati wa kwenda Hospitalini kwa ajili ya mafunzo kwa
vitendo.
1 Pia Serikali imefanikiwa kufikisha
Waraka kwa SUMATRA kuomba magari yafike Chuo cha Afya, waraka ambao SUMATRA
ilijibu ikionesha imeridhia kuhamisha Kituo cha mwisho kutoka CoED na kupeleka
CoHS, na kufanya usajili upya wa magari kufika CoHS mara wamiliki wa magari
wanapoenda kufanya usajili upya wa magari/leseni zao. Ahadi ya SUMATRA ikiwa ni
kutekeleza mpango huu kuanzia Julai 2014
(Mazungumzo
ya mezani ufuatiliaji ulipofanywa na Raisi wa College, Shirikisho na Mwenyekiti
wa Kikao cha Masuala ya Wanafunzi-UDOM, Mbunge wa Kilwa, Mhe. Mangungo June 4,
2014)
F. WIZARA YA FEDHA, KATIBA NA SHERIA
1.
Serikali imefanikiwa kukusanya ada ya
UDOSO, na kurekodi vizuri takwimu za ukusanyaji.
2. Serikali imefanikiwa kulipa posho za
vikao vya viongozi ikiwa ni Baraza la Mawaziri, Bunge na Viongozi katika vituo
vya Tumbi na Iringa kwa mujibu wa bajeti iliyoandaliwa na serikali na kupitishwa
na Bunge.
3. Serikali imefanikiwa kuendesha wizara
zake na ofisi zake zote. Hii ikiwa ni pamoja na kununua vifaa mbalimbali ndani
ya wizara na ofisi hizo kama inavyooneshwa na taarifa za wizara na ofisi
husika, kwa mujibu wa bajeti.
4.
Serikali imefanikiwa kulipa posho kwa
miezi 10 kwa Viongozi wa juu (Makamu wa Raisi, Makamu Msaidizi wa Raisi, waziri
Mkuu na Katibu Mkuu)
G. OFISI KUU
1 Imesimamia utekelezaji wa mipango
mbalimbali ya Serikali kupitia Wizara zake, na kusimamia nidhamu ya viongozi.
2 Ofisi imejenga uhusiano mzuri kati ya
Wanafunzi, Viongozi na Utawala wa chuo CoHS na UDOM.
3 Ofisi ilifanikiwa kupata Viongozi katika
Vituo vya Tumbi na Iringa
4 Serikali imefanikiwa kufungua BlogSpot
ya UDOSO CoHS ili kuboresha mawasiliano kati ya Wanachama wakati wa masomo na
wakati wa likizo.
5 Ofisi imesimamia amani na utulivu kwa
kipindi chote cha kazi na imesimamia na kutekeleza utatuzi wa matatizo na
changamoto mbalimbali kwa kufanya mazungumzo na mamlaka au ofisi husika pasipo
kukiuka utaratibu au kuruhusu vurugu za aina yoyote chuoni.
6 Imefanikiwa kuwakilisha vyema UDOSO CoHS
ndani na nje ya Chuo.
7 Imefanikiwa kufungua UDOSO Blogspot: udosochas.blogspot.com. kwa ajili ya kuboresha mawasiliano kati ya
Wanafunzi na uongozi wao muda wote.
Mwisho wa Mafanikio ya
Serikali CoHS 2013/14
CHANGAMOTO
Kutokukuwepo kwa ushirikino mzuri kati
ya Serikali na Bunge lake katika miezi ya mwisho ya uongozi, na hii ni kutokana
na baadhi ya Viongozi wa Bunge na Wabunge kutofuata njia sahihi ya kushughulika
na Changamoto za hapa na pale.
o Kuwepo na mapato kidogo ya kuendesha
Serikali hivyo kukwamisha baadhi ya mipango na kuleta mvutano katika uongozi
wakati mwingine.
o Usafiri bado ni Changamoto hasa siku za
weekend na nyakati za jioni.
o Wakati mwingine baadhi ya Ofisi za
uongozi wa Chuo kutotoa ushirikiano kwa wakati pale zinapopokea changamoto
zitokazo kwa wanafunzi, hali inayofanya baadhi ya matatizo kuwa ya kudumu.
Mfano;
1. Wakati
mwingine Wanafunzi kuchelewa kupata pesa baada ya kusaini.
2. Funguo
za Vyumba Hosteli za CoHS kutokutolewa kulingana na idadi ya wakazi, hali
inayofanya ufunguo mmoja kutumiwa na watu 4.
3. Baadhi
ya Waalimu kutokuwa wepesi kuelewa changamoto za kitaaluma zinazofikishwa kwao
na wanafunzi.
MAPENDEKEZO
o
Viongozi waheshimiane na wajifunze
kutumia njia sahihi na kusikilizana katika kushughulikia Changamoto za hapa na
pale.
o
Chanzo kingine cha mapato kitafutwe.
o
Majibu na ahadi ya SUMATRA iendelee
kufuatiliwa.
o
Ofisi za uongozi wa Chuo zitoe
ushirikiano kwa wakati pale zinapopokea changamoto zitokazo kwa wanafunzi.
o
Viongozi waendeleze na wadumishe
ushirikiano na uhusiano mzuri kati ya Wanafunzi na Utawala.
o
Serikali ijayo idumishe amani, izuie
vurugu na iwajengee wanafunzi mazingira bora ya kujisomea na kutimiza njozi
zao.
MAMBO
YANAYOHITAJI KUSHUGHULIKIWA MAPEMA NA UONGOZI UNAOINGIA MADARAKANI
1. Ukarabati
wa makazi ya Wanafunzi wa CoHS walioko CoED; milango ya mabafu na vyoo, na
kuzibuliwa kwa vyoo ambavyo vimeziba Block F & G.
2. Kufuatilia
pesa za field BScN 4, Kwa haraka sana maana muda wa field hii umefika, ni mwezi
huu wa June, na kuendelea kufuatilia field za BScN3, Md2 na MD 4-Elective
Research.
3. Kupata
Viongozi katika vituo vya Tumbi Na Iringa.
HITIMISHO;
Mwenyezi Mungu awabariki sana Mawaziri kwa kazi
kubwa Waliyofanya. Pia asaidie Uongozi ujao, katika kutekeleza majukumu yake.
Wanafunzi Ahsanteni, toeni ushirikiano kwa uongozi unaoingia madarakani.
Sameheni serikali kwa maudhi yoyote, Tayari
imekwisha kumsamehe yeyote kwa kosa lolote.
VITU
VINAVYOKABIDHIWA UONGOZI WA UDOSO 2013/14 KWA UONGOZI WA 2014/15
NAMBA
|
OFISI/WIZARA
|
VIFAA
VINAVYOKABIDHIWA
|
01
|
Raisi
na Makamu wa CoHS
|
Mhuri
-1wa Raisi, File 1Kubwa, 3-ndogo, stampad -1, Punching machine -1.
Udosochas.blogspot.com,
Katiba ya UDOSO 2009
|
02
|
Waziri
Mkuu
|
Mihuri
-2 Tumbi &Iringa, stampad -2,Punching machine -1
|
03
|
Katibu
Mkuu
|
Files
4 (2-kubwa, 2-ndogo), Marker pens 1-Box, Staples 1-Set, Office glue ½ Bottle,
Ream Paper-1/2 and 1- Stapler Machine.
Mhuri
-1, stampad -1, Punching machine-1, Kufuli 2 za ofisi
|
04
|
Wizara
ya Fedha, Katiba na Sheria
|
File
-1, 1-Markerpen, eceipt Books 24 (2-Minister, 20-Federal, 2- Iringa &
Tumbi) Cheque Book-1, Bank A/c; UDOSO CHAS A/C No; 0150221581000
|
05
|
Wizara
ya Mikopo
|
Files-2,
Marker- 2.
|
06
|
Wizara
ya Afya na Chakula
|
File-1,
Correction fluid-1,Staple pins.
|
07
|
Wizara
ya Makazi
|
Files-2,
Marker pen -2, Stepla machine -1 &Correction fluid-1bttl
|
08
|
Wizara
ya Michezo, na
|
DSTV
complete except stablizer
|
Football
jersey(CRDB,PPF &LAPF)
|
||
Netball
jersey(PPF)
|
||
Bips
|
||
Four
football
|
||
Three
netball
|
||
Two
pump
|
||
Ministry
file
|
||
Netball
dips
|
||
Football
nets
|
||
Filimbi
|
||
Vijazio
vitatu
|
||
Pump
mbili
|
||
Gloves
for Goalkeeper -1pair
|
||
09
|
Wizara
ya Elimu
|
Dusters
12
|
Rubbed
marker pen -6
|
||
Unrubbed
marker pen -2,
|
||
Spirit
bottles 6
|
||
Ream
paper 1
|
||
File
1
|
||
Punch
machines-1.
|
IMEANDALIWA NA KATIBU MKUU, UDOSO CoHS
OMARI BATULI
SIGN
__________
SIMU: +255-712-127-802
UTHIBITISHO;
Wadhifa; Waziri Mkuu CoHS Wadhifa; RAIS- UDOSO CoHS 2013/14
Jina; Sospeter Mkangi Jina;
ABAYO ASUBUHI Barua
pepe: sospetermkangi@yahoo.com Barua pepe:
abayoasubuhi@gmail.com
Simu:+255-789-752-173 Simu; +255-754-678-845
Imesainiwa Imesainiwa
MAKABIDHIANO YANAFANYIKA LEO Juni 1,2014 KATI YA;
Rais wa Chuo cha Sayansi za Afya 2013/14 na Rais wa Chuo cha Sayansi za Afya 2014/15
Jina: Mhe. ABAYO ASUBUHI Jina: Mhe.
Renatus Mathias
Imesainiwa
Imesainiwa
Makamu wa Rais CoHS 2013/14 Makamu wa
Rais CoHS 2014/15
Jina: Petro Mathias , Imesainiwa Jina: Lyimo
Victoria, Imesainiwa
SHUHUDA; KIKAO CHA SAC, June 1, 2015.
SAINI YA KATIBU WA KIKAO, Imesainiwa
SAINI YA MWENYEKITI
WA KIKAO, Imesainiwa
No comments:
Post a Comment