TANGAZO KWA UMMA
7 September, 2014
YAH: KUJIUZULU KWA KA TIBU MKUU WA
SERIKALI YA WANAFUNZI NA KUVUNJWA KWA
WIZARA YA MICHEZO NA HUDUMA ZA JAMII.
NDUGU WANAFUNZI WA CHUO CHA SAYANSI ZA AFYA NAPENDA
KUWATANGAZIA KUWA OFISI YA RAIS ILIPOKEA BARUA YA KUJIUZULU
KUTOKA KWA KATIBU MKUU WA SERIKALI YA WANAFUNZI TAREHE
30/07/2014 IKIWA INATOA TAARIFA YA KUJIUZULU , SABABU KUU YA
KUJIUZULU NI KUSHINDWA KUWAJIBIKA IPASAVYO KATIKA NAFASI HII
HUKU AKIENDELEA NA SHUGHULI YA MASOMO. HIVYO KWA MUJIBU WA
KATIBA YA UDOSO CHAPTER TWO,PART 1,14(4)b INAMP A MAMLAKA RAIS
KUTEUA KATIBU WA SERIKALI NA PIA CHAPTER TWO PART 1,16(5) KATIBA
INATOA MAELEKEZO JUU YA KUJIUZULU KWA KATIBU KUWA MOJA KWA
MOJA NAFASI HIYO INAKUWA WAZI PIA CHAPTER TWO, PART 1,16(6)(C)
KATIBA INAELEZA KUWA KATIBU ATASHIKILIA NAFASI YAKE MPAKA PALE
ATAKAPO JIUZULU. HIVYO BASI OFISI YA RAIS INAPENDA KUWATAARIFU
KUWA MH SELEMANI MBANGULA KUANZIA TAREHE 31/07/2014 YUKO
NJE YA OFISI
.
WIZARA YA MICHEZO NA HUDUMA ZA JAMII
NDUGU WANAFUNZI WENZANGU NAWATAARIFU KUWA WIZARA YA
MICHEZO IMEVUNJWA RASIMI TAR 7/08/2014.
HIVYO BASI:-
WAZIRI WA MICHEZO: MOSHA HENRY G.
NAIBU WAZIRI :MUSTAPHA ADAM
HAWATA KUWA VIONGOZI KATIKA WIZARA HII:
NDUGU WANAFUNZI SABABU ZA KUVUNJWA KWA WIZARA HII NI KAMA
IFUATAVYO:
1;KUTOWEPO KWA MAELEWANO YA
KIUTENDAJI BAINA YA VIONGOZI WA WIZARA HII
IMESABABISHA WIZARA KUSHINDWA KUFANYA KAZI KWA UFANISI
UNAOTAKIWA.
2; KUSULUHISHWA KWA VIONGOZI KATIKA WIZARA HII MARA
KADHAA NA KUPEWA MWONGOZO WA KAZI BILA MAFANIKIO.
3;KUDHARAU MAAMUZI YA BARAZA LA MAWAZIRI YA TAREHE
18 JULAI 2014, JUU YA KUKUTANA NA VIONGOZI WA PANDE ZOTE
MBILI STASHAHADA MWAKA WA KWANZA NA SHAHADA MWAKA
WA KWANZA ILI KUTAFUTA SULUHU JUU YA VURUGU ZA MCHEZO
WA FAINALI MPIRA WA MIGUU, MBUZI CUP ,ILIO FANYIKA JULAI
11 ,2014 .
4; KUJIUZULU KWA NAIBU WAZIRI KATIKA WIZARA HII, MNAMO
TAREHE 20 JULAI 2014, OFISI YA RAIS IMEPOKEA BARUA YA NAIBU
WAZIRI KATIKA WIZARA HII AKIMTAARIFU RAIS JUU YA
KUSHINDWA KUENDELEA KUTUMIKIA UMMA KUPITIA WIZARA HII.
KUTOKANA NA SABABU 1,2,3,&5 ZILIZOTAJWA HAPA.
5; WIZARA KUSHINDWA KUWAKUTANISHA WADAU WA SOKA
KWA PAMOJA ILI KUPATA UTATUZI WA CHANGAMOTO ZA
KUTOKUELEWANA BAINA YA WADAU HAO; IKUMBUKWE KUWA
HALI HII YAWEZA KUJENGA UHASAMA MKUBWA.NA KUVURUGA
HALI YA KIMICHEZO CHUONI KWETU
KWA HALI HII BASI;
KWA MUJIBU WA KATIBA YA SERIKALI YA WANAFUNZI YA MWAKA 2007
ILIYO FANYIWA MAREKEBISHO MWAKA 2009, CHAPTER TWO, PART I, 14 (4)(b)
INAMPA MAMLAKA RAIS YA KUCHAGUA WAZIRI AMA NAIBU WAZIRI
KATIKA WIZARA HUSIKA.
PIA SEHEMU YA KATIBA YA SERIKALI YA WANAFUNZI ,CHAPTER TWO , PART
I ,16F (3)(b), INAMPA RAIS MAMLAKA WA KUMWONDOA WAZIRI AMA
NAIBU WAZIRI KUTOKA KATIKA WIZARA LAKINI PIA CHAPTER TWO,PART
I, 16F(3)(a) INAELEZA NAFASI YA KIONGOZI WA WIZARA YAWEZA BAKI WAZI
ENDAPO KIONGOZI WA WIZARA AKIFA AU KUJIUZURU.
NIMEAMUA KUIVUNJA WIZARA HII NA KUUNDA UONGOZI MPYA AMBAO
UTAFANYA KAZI KWA KIPINDI KILICHO BAKI.
RAI YANGU KWENU WANAFUNZI WENZANGU, TUWE WATULIVU
TUDUMISHE AMANI YA CHUO CHETU ILI KUJENGA JAMII YENYE UPENDO
NA USHIRIKIANO/MSHIKAMANO MZURI.
N.B MABADILIKO KATIKA WIZARA HII YATATANGAZWA .
IMETOLEWA NA;
…………………………..
MATHIAS RENATUS
Rais:- chuo cha afya
Thursday, October 9, 2014
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment