UDOSO CHAS –UDOM
TAARIFA KWA WANAFUNZI
WOTE WA TIBA
UONGOZI WA WANAFUN ZI TIBA UNAPENDA
KUWAJULISHA
YAFUATAYO;
1.
USAFIRI
Ndugu wanafunzi kwanza na ijulikane kuwa
changamoto ya usafiri tumeona tangu tumepata taarifa ya idadi ya wanafunzi
wanaopokelewa na chuo chetu. Baada ya hapo tumefanya jitihada za kushughulikia
suala la usafiri kama ifuatavyo;
Mpaka
sasa tumeongea na uongozi wa Chuo ili tuongezewe idadi ya magari ya chuo ya kutuchukua
toka Education kwenda Tiba, Uongozi wa chuo mwanzoni walitujibu hilo ni suala lisilowezekana
Kwani Magari yote ni kwa ajili ya Stafu tu Lakini leo pia Imebidi niende asubuhi saa
Tatu nilikuwa Ofisini hapo na nimetoka saa sita Central administration kuongea na Viongozi mbalimbali
na Wote kwa pamoja, wamenisikiliza na wamekubali niwape Barua yangu na wameniahidi
kufanyia kazi maombi hayo na kesho nitarudi tena ili kujua wanasemaje zaidi kuhusu
Maombi haya! Nadhani ni hatua nzuri hii zaidi mniombee ili Mafanikio
yapatikane. Kesho nitarudi
tena na nitakuwa na taarifa nyingine kesho tofauti na hii. Vumilieni Msinung’unike!
PILI
Wiki
jana tulienda SUMATRA kushughulikia suala la usafiri ili tupate magari ya kuja
Tiba na
MKurugenzi wa SUMATRA aliahidi kuwa Jumanne ya 22.10.2013 yaani Leo
atafanya kikao na
wenye
Daladala wote na kesho Jumatano atatupa majibu, aidha tulimpa pendekezo la Kuvunja
kituo
cha Education ili mwisho wa Magari uwe ni Tiba na Traffic awepo Education ili kuzuia
magari yasiishie pale. Alikubali kuwa atafanyia kazi hayo
mapendekezo na kesho tutapata majibu yake
, naomba tuvute subira kidogo, Kesho ni karibu! Vumilieni Msinung’unike!
Wakati Tukisubiri Tufanye
Nini?
Kesho tutembee au tupande pikipiki na wengine tukapande
magari yatakayofika. No anymore answer I can give you this time. I want to be
realistic!
BUMU
Tunapenda kuwataarifu kuwa taarifa kamili zinaonesha Pesa za Meal, Accommodation & Books and
stationary allowances hazijafika chuoni kutoka HESLB nayo
bodi pia inakiri.
Tutegemee nini
sasa?
Kwa hiyo basi tutambue kuwa “subira yavuta heri” Nawaombeni tuvute subira tuone hizo hali
inaendeje mpaka mwisho wa wiki hii na mwanzo wa wiki kesho kama mambo yatakuwa
hayajaeleweka Jumatatu Tutaenda Daresalaam! Vumilieni Msinung’unike!
MIZIKI VYUMBANI
Wana Tiba mnaombwa
kupunguza sauti za miziki Vyumbani, taratibu za Vyuo haziruhusu, Msije mkapata
matatizo Please.
Nawatakia uelewa na
utekelezaji mwema. Ahsanteni sana!; TAARIFA IMECHELEWA KWA SABABU MTANDAO HAUKUWA NA NGUVU.
No comments:
Post a Comment